Monday, 27 June 2016

Zifahamu faida za mwarobaini

Mwarobaini ni mti maarufu sana na unajulikana karibu kila mahali , huku ukielezwa kuwa mti huo ni kati  ya miti mirefu yenye ukijani mzuri sana, ingawaje majani yake ni machungu mno.
Mti huo umekuwa ukifahamika kwa uwezo wake wa kusaidia magonjwa ya aina mbalimbali, huku ikiaminika kwamba  mti huo asili yake ni nchini India.
Pia mwarobaini hustawi zaidi katika nchi za ‘tropic’ na una uwezo mkubwa  wa kuhimili hali ya ukame.  
Kwa hapa nchini, mti wa mwarobaini huweza kupatikana kwa urahisi kabisa katika maeneo mengi ya mijini na vijijini pia.

Jina la mti huu mwarobaini linatokana na imani kuwa mti huu una uwezo wa kusaidia magonjwa yapatayo arobaini, huku majani yake na mbegu zikitumiwa kama tiba kwa miaka.
Mtaalam wa tiba asili hapa jijini Dar es Salaam Dk Abdallah Mandai, anasema kwamba magome ya mti wa mwarobaini yakichemshwa huwa ni dawa ya kuua minyoo yote tumboni, homa, kikohozi na kujisikia kuwaka moto, kuharisha pamoja na tatizo la vidonda vya tumbo.
Unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallah Mandai kwa ushauri zaidi juu ya mpangilio wa mlo wako piga simu namba +225 716 300 200/+225 784 300 300/+225 769 400 800 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.comaNo comments:

Post a Comment