Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 8 June 2016

Zifahamu hizi faida za msingi kiafya utakazo zipata ukitumia nyanya

NYANYA ni moja ya tunda, lakini pia ni kiungo ambacho wengi wetu tumekuwa tukikitumia katika kuungia mboga ili kuongeza ladha ya chakula

Zipo faida kadhaa za kutumia nyanya kama tunda miongoni mwa faida hizo ni pamoja na:

Kuimarisha uoni wa macho, nyanya inaweza kusaidia kuongeza ufanisi wa uoni wa macho kutokana na kuwa na vitamin A ambayo pia husaidia kuepuka tatizo la kutoona vizuri usiku night –blindness.

Nyanya pia huimarisha afya ya damu ndani ya mwili, hii ni kwasababu ndani ya nyanya kuna madini ya chuma ambayo husaidia kurekebisha afya ya damu mwilini.

Pia ndani ya nyanya kuna Vitamin K ambayo ambayo husaidia kudhibiti kutokwa kwa damu na kusaidia mzunguko wa damu ndani ya mwili.

Nyanya husaidia kulinda afya ya moyo, matumizi ya kiungo hiki huimarisha kiwango cha cholesterol kwenye damu . Hii ni kutokana na kuwa na kirutubisho kiitwacho ‘lycopene’.

Mbali na faidia hizo pia matumizi ya mara kwa mara ya nyanya husaidia kuboresha umeng’enyaji wa chakula ndani ya tumbo na hivyo kusaidia kutatua changamoto ya ukosefu wa choo, lakini pia hata tatizo lakuhara.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallah Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment