Monday, 20 June 2016

Zifahamu hizi faida za tongo

 
Leo tunazungumzia faida ya tango katika miili yetu, ni wazi kwamba tunda hili wengi wetu tumekuwa tukilitumia sana lakini hatufahamu umuhimu wake ndani ya miili yetu.

Kuna matunda mengi na yenye ladha nzuri na tamu, lakini kwa tango si tunda lenye ladha tamu, lakini umuhimu wake unaonekana zaidi baada ya kuingia mwilini.

Tango ni chanzo kizuri cha vitamin B na linauwezo wa kuupatia mwili nguvu pia.

Tunda hili pia husifika kwa uwezo wake wa kuimarisha afya ya ngozi, ambapo mhusika huweza kutumia kwa kusugulia kwenye ngozi taratibu na likaleta matokeo mazuri kwa ngozi ya mhusika.


Tango husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani, lakini pia linauwezo wa kuondoa ‘hangover’ kwa watumiaji wa pombe kwani lina vitamin B ambazo husaidia kupunguza ukali wa maumivu

Husaidia afya ya viungo, huondoa ‘gout’ na ugonjwa wa baridi yabisi ‘Arthritis’ tango ni chanzo kizuri cha ‘silica’ ambayo inafahamika kusaidia afya ya viungo kwa kuimarisha viunganishi vya viungo ‘connective tissue’ pia  lina Vitamin A, B1, B6, C & D, ‘Folate’ ‘Calcium’ Magnesium na ‘potassium’ husaidia

Kwa maelezo zaidi na ushauri wasiliana na  Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment