Saturday, 25 June 2016

Zifahamu hizi sifa za fenesi kwa afya yako

Fenesi ni miongoni mwa matunda ya msimu yenye umbo la pekee na ladha tamu ya aina yake.

Tunda hili linaingia kwenye orodha ya matunda ambayo yanatajwa kuwa na faida nyingi kiafya katika mwili wa mwanadamu.
 
Kula gramu 100 tu ya fenesi huweza kuupatia mwili nguvu ya kalori 95, na tunda hili lina nyama laini iliyojaa sukari aina ya 'fructose' na 'sucrose' inayoweza kuupatia mwili nguvu.

Aidha, fenesi limejaa ufumweli au fibre, sifa inayosaidia kulainisha choo vile vile tunda hili lina virutubisho kadha wa kadha vyenye faida kubwa mwilini. 

Baadhi ya virutubisho hivyo ni vitamini A, C, B 'complex' vitamin B6, 'folic' 'acid' 'niacin' 'riboflavin' na madini za aina mbalimbali kama vile 'potassium' 'magnesium' 'manganese' na chuma. 

Katika tunda la fenesi kuna 'protini' mafuta, wanga na 'antioxidants'.

Mbali na hayo, fenesi pia linatajwa kuwa chanzo kizuri cha nishati kisichokuwa na mafuta. Si hayo tu, bali pia kwa kuwa na virutubisho vyenye uwezo wa kuondosha sumu mwilini, tunda hilo linaweza kuukinga mwili dhidi ya saratani na magonjwa mengine na pia kuongeza uwezo wa kuona

Unaweza kuwasiliana nasi kwa mawasiliana yafuatayo: +255 716 300 200/ +255 754 391 743/ +255 784 300 300 Barua pepe, dkmandaitz@gmail

No comments:

Post a Comment