Wednesday, 29 June 2016

Zitambue faida za alo vera kiafya zaidiAlo vera ni mmea unaopatikana porini na unafanana sana na mmea wa katani na una miiba pembeni, lakini kuna aina nyingi ya mmea huu isipokuwa hapa nataka kuzungumzia ile alovera ambayo ni chungu. 

Mmea huu unasifika kwa kutoa msaada wa kutuliza maradhi mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchungu wake, miongoni mwa magonjwa hayo ni pamoja na malaria, kuumwa na wadudu, baridi yabisi.

Alo vera pia huleta hamu ya kula na husaidia mmeng'enyo wa chakula tumboni sambamba na kuwasaidia wale wenye matatizo ya shida ya haja ndogo mkojo kutoka kwa shida.

Aidha, magonjwa mengine ambayo huweza kutibika kwa kutumia alo vera ni pamoja na shinikizo la damu la juu, saratani ‘cancer’ bawasira, mkanda wa jeshi na kusaidia askari wa kulinda mwili.

Pamoja na hayo, inaelezwa kuwa alo vera nayo husaidia kuongeza nguvu za kiume na kuwasaidia wale wenye shida ya kuvimba mwilini.

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuongea na Tabibu Abdallah Mandai kupitia simu namba +255 716 300 200/+255 784 300 300/+255 769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment