Monday, 18 July 2016

Chai ikiwekwa viungo hivi husaidia kuondoa maumivu ya viungo mwilini


Miongoni mwa matatizo ambayo huwakumbuka watu wengi ni pamoja na hili tatizo la maumivu ya viungo mwilini.

Leo napenda tufahamu hivi viungo vya chai viwili ambavyo huweza kusaidia kupunguza tatizo hilo, lakini pia nimekuongezea njia nyingine mbili ya kutumia binzari na maji ya baridi.

Tangawizi
Kiungo hiki ni muhimu pia kwa kupunguza maumivu ya viungo mwilini kutokana na kiungo hicho kuwa na uwezo wa kurahisisha mzunguko wa damu kwenda vizuri ndani ya mwili. Hivyo matumizi ya kikombe kimoja cha tangawizi kila siku huweza kuwa msaada kwako ikiwa unatatizo la maumivu ya viungo.

Mdalasini
Kama una maumivu ya viungo pia unaweza kutumia kiungo hiki ambapo unaweza kunywa maziwa yalichanganywa kidogo na mdalasini pamoja na asali kidogo na utaona faida yake.

Binzari
Kiungo hiki kinafahamika sana kwa akina mama na wengine hukifahamu kwa jina la manjano, ili kiungo hiki kiwe msaada kwa tatizo hili utahitajika kupata maziwa kisha changanya na kijiko kidogo cha binzari baada ya hapo chemsha kwa pamoja kisha subiri yapoe kiasi, lakini yasipoe kabisa halafu utatumia pamba kuchua sehemu yenye tatizo.

Matumizi ya maji ya barua
Moja ya njia ya kupambana na maumivu ya viungo mwilini ni pamoja na kuoga maji ya baridi ambayo husaidia kuiamsha misuli ndani ya mwili na kupumnguza maumivu ya viungo vya mwili.

ZINGATIA
Ni muhimu kuwasiliana nasi kwa maelezo zaidi juu ya matumizi ya viungo hivyo ili kupata matokeo mazuri zaidi. Unaweza kutupigia simu sasa kwa namba +255 716 300 200/ +255 784 300 300/ +255 769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.No comments:

Post a Comment