Tuesday, 19 July 2016

Fahamu hivi vyakula na matunda vinavyosafisha mishipa damuMatatizo ya mishipa ya damu kuziba ni moja ya matatizo yanayochangiwa na kuishi maisha ya kubweteka pasipo kuwa na mazoezi.

Tatizo hili mara nyingi huwapata wanawake zaidi kuliko wanaume, katika nchi zinazoendelea inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 30 ya wanawake na asilimia 10 ya wanaume wanaofika hospitali hukabiliwa na maradhi hayo.

Vifuatavyo ni vyakula na matunda ambavyo huweza kusaidia kusafisha mishipa ya damu.

Parachichi
Avocados
Tunda hili imesheheni virutubisho vingi vyenye manufaa kiafya ikiwa ni pamoja na kupunguza cholesterol kwenye mishipa ya damu.

Korosho/ Karanga
Nuts
Vyote viwili hivi  husaidia kupunguza tatizo hilo kwani ndani yake vina kirutubisho cha Omega- 3,  pamoja na nyuzinyuzi na vitamin E ambazo kwa pamoja husaidia husaidia kulinda afya ya moyo. Omega 3 husaida kuondoa cholesterol ndani ya mishipa ya damu.

Komamanga
Pomegranate
Pia ni miongoni kati ya matunda ambayo husaidia kusafisha mishipa ya damu mwilini kutokana na kuwa na kirutubisho cha 'antioxidants' ambacho husaidia kusafisha mishipa ya damu hasa inapotumika juisi yake zaidi.

Manjano/binzari
Turmeric
Hiki ni kiungo ambacho nacho kinauwezo wa kusaidia kusafisha mishipa ya damu pale kinapotumika vizuri.

Broccol
Broccoli
Hii ni aina ya mboga fulani za majani ambayo mara nyingi hutumiwa na wahindi zaidi, lakini ndani yake ina vitamin K ambayo ni muhimu kwa afya ya mifupa mwilini na kuzuia calcium kuharabi mishipa ya damu.Pia husaidia kushusha kiwango cha  'cholesterol'

Kwa kufahamu zaidi kuhusu masuala ya lishe na mimea tiba unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200, +255 784 300 300, +255 769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment