Thursday, 28 July 2016

Fahamu namna ya kutumia aloe vera kumaliza michirizi ya kwenye ngozi

Michirizi kwenye ngozi ni ile hali ya kutokea alama za mistari kwenye ngozi na mara nyingi hutokea baada ya mabadiliko ya mwili ya ghafla kama kunenepa, kunyanyua vyuma, kubeba mimba na kadhalika.

Alama hizo huwa hazina madhara, lakini huwa hubadili ngozi ya mhusika na kuifanya kutoonekana vizuri, hivyo huwa kero kwa mhusika.

Leo napenda kukufahamisha hizi mbinu nyingine za kumaliza tatizo hilo kwa kutumia vitu ambavyo vinakuzunguka katika maisha yako ya kila siku.

Matumizi ya Aloe Vera
Mmea huu umekuwa ukipatikana maeneo mbalimbali hapa nchini na umekuwa ukitumiwa na jamii mbalimbali kwwa kutibu matatizo mbalimbali vikiwemo vidonda na ngozi.

Sasa ili utumie mmea huu kwa kuondoa michirizi mwilini mhusika atapaswa kupata sehemu ya majani ya mualovera kisha atahitajika kupaka sehemu iliyoathirika kisha kukaa nayo ndani ya dakika 10 hadi 15 na baadaye kuosha.

Unaweza kuwasiliana nasi kwa maelezo zaidi tupigie simu sasa kwa namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment