Saturday, 16 July 2016

Fahamu namna ya kufukuza mbu kwa kutumia tango na limao


Malaria ni miongoni mwa magonjwa ambayo yamekuwa yakichangia vifo vingi vya kinamama wajawazito pamoja na watoto husani wenye umri chini ya miaka mitano.

Kimsingi ugonjwa huu umekuwa ukisababishwa na kuumwa na mbu jike aitwaye 'anopheles'

Njia nyingi zimekuwa zikitumika katika kupambana na mbu huyo (anopheles) miongoni mwa njia hizo ni pamoja na kutumia vyandarua kabla ya kulala, kufanya usafi maeneo yanazunguka mkazi, pamoja na kutumi dawa za kupaka na kupuliza ambazo harufu yake husaidia kufukuza mbu hayo.

Sasa leo napenda kukushirikisha njia hizi za asili za kutumia matunda ambayo yanapatikana katika mazingira yetu ya kila siku njia hii naamini itakakusaidia kupambana na mbua hao.

Matango
Matumizi ya tunda hili la tango huweza kusaidia kufukuza mbu wanaosababisha maambukizi ya malaria, kinachotakiwa kufanya ni kukata vipande vya mduara (round) vya tunda hilo kisha paka sehemu zote za mwili ambazo zitakuwa wazi baada ya hapo utaweza kulala au kuendelea kutazama tv sebuleni bila kupata usumbufu wa kuumwa na mbu tena. Kama utakuwa umekata vipande vingi vya tango unaweza kuvihifadhi kwenye barafu au friji kwa matumizi ya siku inayofuata tena

Limao
Unaweza pia kutumia limao kama utakuwa umekosa tango, ambapo utahitajika kukata viapnde vya limao kisha sugua taratibu sehemu za mwili za wazi na kipande hicho. AU unaweza kukamua juisi ya limao kisha chukua pamba na utachovya kwenye maji hayo ya limao kisaha kupaka sehemu za mwili na utaona matokeo mazuri ya kutozongwa na mbu tena.


Kwa mengine mengi kuhusu matumizi ya mimea tiba kwa faida zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 784 300 300/ +255 769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Zingatia
Usiache kulala bila kushusha chandarua (net) ili kuwa salama zaidi dhidi ya mbu waenezao malaria
No comments:

Post a Comment