Monday, 25 July 2016

Fahamu orodha ya vyakula na matunda vinavyoweza kulinda afya tumbo


Matatizo ya kuwa na umeng'enyaji wa chakula mbovu huchangiwa na  mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vyakula vyenye asili ya nyuzinyuzi pamoja na maji.

Mara nyingi tatizo hili limekuwa likichangia tatizo la ukosefu wa choo, hayo ndio tunaweza kusema madhara ya kuwa na mmeng'enyo mbovu wa chakula.

Leo napenda kukufahamisha hii orodha fupi ya viungo, matunda na vyakula ambayo husaidia kurekebisha umeng'enyaji wa chakula tumboni.

Viazi vitamu

Viazi hivi vimesheheni wingi wa nyuzinyuzi ambayo huhitajika sana katika kuboresha umeng'enyaji wa chakula tumboni, lakini viazi hivi pia vinapotumika vizuri huweza kuwasaidia hata wale wenye matatizo ya vidonda vya tumbo.

Parachichi

Tunda hili nalo lina kiwango cha nyuzinyuzi pamoja na mafuta mazuri ndani yake ambayo nayo ni msaada tosha wa kuboresha mfumo mzima wa umeng'enyaji chakula tumboni.

Tangawizi


Tangawizi ina asilimia kubwa zaidi ya kurekebisha mfumo mzima wa umeng'enyaji wa chakula ndani ya tumbo kwani kiungo hiki nacho kimesheheni nyuzinyuzi za kutosha ndani yake.

Apple /Tufaa

Ndani ya tunda hili pia kuna nyuzinyuzi ambazo huwa msaada kwa mfumo wa umeng'enyaji chakula, lakini pia tunda hili linafaa zaidi endapo utakula pamoja na maganda yake.

Ndizi mbivu

Pia ni tunda ambalo lina nyuzinyuzi za kutosha ambazo huenda kufanya kazi ya kurekebisha umeng'enyaji wa chakula tumboni.

Kwa kufahamu mengi zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 784 300 300/ +255 769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment