Saturday, 2 July 2016

Fahamu umuhimu wa majani ya parachichi kiafya


PARACHICHI ni miongoni mwa matunda yenye ladha nzuri na ni maarufu duniani kote. Kutokana na utamu na wingi wake wa mafuta, unaweza kudhani siyo tunda zuri kiafya, lakini ukweli tunda hilo ni msaada mkubwa kwa binadamu.

Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa watu wenye mazoea ya kula tunda hilo kwa wingi huwa na afya njema na uzito unaokubalika kiafya.

Tunda hilo lenye mafuta mengi, wingi huo unasaidia kupunguza hatari ya mtu kupatwa na kiharusi au ugonjwa wa moyo.

Miongoni mwa faida za parachichi ni pamoja na kudhibiti shinikizo la damu, kushusha kiwango cha lehemu ‘Lower Cholesterol Levels’, kudhibiti ugonjwa wa kisukari , kupunguza maumivu ya viungo na magonjwa ya kuvimba pamoja na kuimarisha uwezo wa kuona vizuri.

Katika tafiti ambazo ziliwahi kufanyika huko nyuma nchini Mexico, zinaonesha kuwa ulaji wa tunda la parachichi husaidia kupunguza kiwango cha lehemu mwilini.

Faida nyingine ni pamoja na kuimarisha mifupa ya mwili, kuimarisha usagaji wa chakula tumboni, lakini pia parachichi ni moja ya matunda ambayo hufaa zaidi kuliwa na wajawazito.

Aidha, tunda la parachichi lina virutubisho vya aina mbalimbali, ambavyo ni pamoja na vitamin C , B6, E, K pamoja na madini ya ‘copper’ na ‘potassium.’

Mbali na tunda la parachichi kuwa tiba, pia hata majani ya mparachichi ni tiba ya magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na matatizo ya vidonda vya mdomoni na kuimarisha meno na kupunguza maumivu ya meno.

Majani yake yanapochemshwa kama chai na mtu kunywa husaidia kuondoa matatizo mbalimbali mwilini, kama vile hali ya uchovu, udhaifu, kuumwa kichwa, koo, tumbo, mapafu na uvimbe.

Vilevile majani ya mparachichi yana nafasi ya kumsaidia mwanamke ambaye hupata maumivu wakati wa kipindi cha hedhi, ili yatumike katika tatizo hili mhusika atalazimika kupata majani 6 ya mparachichi na kuyachemsha kwenye maji lita moja na kuyaacha yapoe kabla ya kuanza kunywa.

Majani ya mparachichi pia husaidia kutibu majeraha, ili kufanikiwa katika hili unapaswa kusaga majani hayo kisha mhusika atahitajika kutumia unga huo wa majani ya parachichi kwa kuweka sehemu yenye jeraha kila siku kutwa mara tatu.

Unaweza kuuliza maswali au kutoa maoni kwa simu namba +255716 300 200/ +255769 400 800/ +255784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment