Friday, 8 July 2016

Fahamu undani wa faida za matumizi ya mbegu za papai kiafyaPAPAI ni moja ya tunda lenye ladha nzuri na pia limesheheni wingi wa virutubisho kadhaa na kiwango kikubwa cha maji.

Watumiaji wengi wa tunda hili huishia kula tunda pekee, huku mbegu za tunda hilo zikitupwa hii ni kutokana na kutotambua kuwa mbegu za tunda hilo nazo zinamanufaa kwa afya.

Hapa ninazo baadhi ya faida za mbegu hizo kiafya ambazo ningependa tuzifahamu kwa pamoja:

Hupunguza hatari ya kukumbwa na saratani
Kwa mujibu wa utafiti uliowahi kufanyika mwaka 2004 ulionesha kuwa mbegu hizo zinauwezo wa kutuliza maumivu ya sehemu mbalimbali za maungio mwilini (joint). Utafiti huo uliainisha kuwa ndani ya mbegu hizo kuna kirutubisho kiitwacho ‘antioxidant’ na ‘cytoprotective’, pia ilibainika kuwa mbegu hizo zinautajiri wa ‘flavonoid’. Hivyo basi mbegu hizo zinauwezo wa kumkinga mhusika dhidi ya saratani.

Huimarisha kinga ya mwili
Mbegu hizi pia zinayo nafasi kubwa ya kuimarisha kinga ya mwili na kumfanya mhusika kuwa upande salama dhidi ya magonjwa.

Husaidia kuzuia figo kuharibika
Hii ni kwasababu mbegu hizi huwa na uwezo wa kupunguza sumu mwilini na hivyo kuisaidia figo kuipunguzia kazi ya kuchuja sumu mwilini. Kwa mujibu wa utafiti ulifanywa na Chuo Kikuu cha Karachi kilichopo Pakistan wao walibaini kuwa mbegu hizi za papai zinauwezo wa kupambana na matatizo mbalimbali ya figo ikiwa ni pamoja na kiungo hicho kushindwa kufanya kazi ‘kidney failure’

Hupunguza maambukizi ya virusi

Mbegu hizi za papai husaidia kupambana na maambukizi mbalimbali ambayo huweza kuenezwa kwa njia ya virusi.

Kama utakuwa na swali maoni au ushauri unaweza kutupigia kwa simu namba 
+255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment