Saturday, 23 July 2016

Fanya mambo haya kama unataka kuanza siku yako vizuri


Kunawakati unaweza kujikuta umeamka upo hovyo na utamani kufanya chochote kwa siku hiyo yaani kila kitu kwako unaoni ni kikwazo.

Hali kama hiyo si jambo la ajabu kwa binadamu yoyote na huweza kumtokea mtu yoyote katika maisha. Sasa hapa leo nataka kukwambia baadhi ya mambo ambayo yatakufamya kubadili asubuhi yako na ukajikuta umekuwa mchangamfu tu.

 Anza siku yako mapema.
Jitahidi kuamka mapema zaidi kwani wataalam wa masuala ya saikolojia wanaeleza kuwa asubuhi na mapema ni muda mzuri zaidi ambapo akili inakuwa imetulia na kuweza kufikiri kwa ufanisi zaidi.

Pia unaweza kuutumia muda huo wa kumka mapema kupanga mipango yako ya kazi kwa siku husuka.

Fungua madirisha yako
Unapoamka na kufungua madirisha ya nyumba yako au chumba chako hapo utakuwa umeruhusu mwanga wa jua pia kuingia ndani kwako ambao huusaidia mwili kupata msisimko.

Mwanga wa jua pia ni chanzo kizuri cha vitamin D, lakini husaidia kukuweka kuwa na hali nzuri 'mood'.

Kunywa maji ya limao
Unywaji wa maji haya husuaidia kuimarisha afya ya umeng'enyaji chakula, lakini pia maji hayo ni chanzo kizuri cha vitamin C hivyo husaidia kuimarisha kinga za mwili.

Kuoga
Kuoga mapema nako ni muhimu kwani huufanya mwili kuchangamka na akili pia kuwa vizuri

Soma vitabu vitakavyokutia moyo
Unapoamka asubuhi na kusoma unakuwa tayari umeiandaa akili yako vizuri kupambana na majukumu ya siku hiyo hivyo unaweza kusoma kidogo.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment