Friday, 29 July 2016

Fanya mambo haya kama unatatizo la kuwa na macho mekundu


Habari za leo mdau wangu wa tovuti hii naamini utakuwa upo vizuri, leo nimeona tufahamishane baadhi ya mambo ambayo yatakusaidia wewe mwenye tatizo la mcho yako kuwa mekundu.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo yakizingatiwa husaidia kuboresha afya ya macho.

Ulaji wa matunda na mboga za majani
Mbogamboga na matunda huwa na vitamin muhimu kwa ajili ya macho mfano A,C, na E ambazo kimsingi ndio muhimu sana kwa ajili ya macho.Katika matunda unaweza kutumia tango pia ili kuboresha macho yako zaidi

Kulala kiasi cha kutosha
Wataalam wa masuala ya afya wamekuwa wakipendekeza kuwa binadamu alale angalau saa saba hadi nane kwa siku ili kuurudisha mwili uliochoka katika hali yake ya kawaidi, kwani mtu anayekosa usingizi wa kutosha ni rahisi kwake kuwa na macho mekundu kwa sababu ya uchovu.

Unywaji wa maji mengi sanaKunywa angalau glass 8 mpaka kumi kwa siku ni muhimu sana kwa macho yako kwani maji husafisha mwili wote na kuondoa sumu mwilini. kutokunywa maji huweza kuchangia mwili kuwa mkavu na macho mekundu.

Punguza kazi za macho;
Hii ni kwa wale ambao hufanya kazi za computer au kuangalia movie hali hiyo nayo huchangia kuhchosha macho na hivyo kuweza kuchangia kuwa mekundu.

Epuka matumizi ya pombe kupita kiasi

Epuka mazingira yenye vumbi na moshi


Zingatia
Ni vyema kuwaona wataalam wa macho ikiwa unaona tatizo hilo limeendelea kukusumbua kwa muda mrefu, lakini pia jenga utaratibu wa kuchunguza macho yako angalau mara mbili kwa mwaka kama wataalam wanavyoshauri.

Tunaweza kukushauri kuhusu matumizi ya lishe bora na vitu vya asili tupigie sasa kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment