Wednesday, 27 July 2016

Haya hapa mambo manne yanayoweza kusababisha ugumba kwa wanawake


Ugumba ni hali ya wapenzi au mke na mume kutopata ujauzito baada ya kushiriki tendo la ndoa kwa muda wa mwaka mmoja mfululizo.

Ugumba unaweza kugawanyika katika makundi mawili ambayo ni Primary Infertility yaani mtu hajawahi kubeba mimba kabisa kuzaliwa kwake.

Kundi la pili ni Secondary Infertility yaani mtu ambaye amewahi kuzaa lakini kwa baadaye akajikuta anashindwa kubeba ujauzito.

Zifuatazo ni baadhi ya sababu ambazo huchangia tatizo la ugumba

Utoaji wa mimba
Utoaji mimba una hatari nyingi ambazo huweza kuchangia ugumba ikiwa kizazi kitapata mashambulizi ya bacteria au makovu yanayoletwa na vifaa vinavyotumika kutoa mimba kwenye mfuko wa uzazi.

Matatizo ya mirija ya uzazi
Wakati mwingine mirija hiyo huziba kwa sababu mbalimbali hivyo mayai hushindwa kupita na kusababisha ugumba.

Magonjwa mengine ya mwili
Magonjwa yeyote ya binadamu ambayo huingilia mfumo wa homoni za uzazi huweza kusababisha ugumba.

Msongo mkubwa wa mawazo

Hii nayo ni moja ya sababu ya tatizo hili endapo kiwango cha msongo wa mawazo kitakuwa cha hali ya juu.

Usisite kutuuliza chochote kuhusu hali yako ya kiafya tupigie sasa kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment