Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 4 July 2016

Hivi hapa vyakula na vinywaji vya aina tano vitakavyosafisha figo yako leo


AFYA ya figo ni muhimu kama ilivyo afya ya moyo, hii ni kwa sababu figo ni moja ya kiungo ambacho husaidia kuchuja sumu mbalimbali ndani ya mwili na baadaye kutoa taka mwili kwa njia ya haja ndogo (mkojo)

Matatizo ya figo huweza kuchangia ugumu wa upatikanaji wa haja ndogo (mkojo) au miguu na mikono kuvimba.

Pia mtu mwenye shida ya figo huwa katika hatari kubwa ya kukumbwa na matatizo ya moyo.

Hata hivyo, kuna baadhi ya vyakula na vinywaji ambavyo tunaweza kusema ni vyakula rafiki kwa afya ya figo ndani ya mwili na husaidia kulinda afya kiungo hicho.

Baadhi ya vyakula na vinywaji hivyo ni hivi vifuatavyo;

Juisi ya limao

Ni miongoni kati ya vinywaji ambavyo ni muhimu kwa afya ya figo. Baadhi ya tafiti ambazo zimewahi kufanyika zinaeleza kwamba juisi ya limao pia huweza kuondoa hatari ya kukumbwa na tatizo la mawe kwenye figo endapo juisi hiyo itatumika mara kwa mara.

Matumizi ya juisi
Juisi mbalimbali za matunda nazo zinauwezo mzuri wa kulinda afya ya figo, miongoni mwa matunda ambayo yanashauriwa kutumika katika kulinda afya ya figo ni pamoja na 'apple', nanasi, tango, chungwa pamoja na peazi.

Mboga za majani
Mboga za majani pia husaidia kulinda afya ya figo, mfano wa mboga hizo ni pamoja na spinachi

Kiazi Kikuu (Beetroots Juice)
Kiazi kikuu kinapoandaliwa kama juisi husaidia kupunguza sumu ndani ya mwili,kutokana na hali hiyo figo inakuwa imepunguziwa kazi kubwa ya kuchuja sumu mwilini na kuifanya figo kuendelea kubaki na afya njema.

Kunywa maji ya kutosha
Unywaji wa maji ya kutosha mara kwa mara ni moja ya njia ya kulinda afya ya figo yako, hivyo ni vizuri kuzingatia kunywa maji ya kutosha kila siku angalau yasiyopungua glasi 8.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.comNo comments:

Post a Comment