Monday, 18 July 2016

Hivi ndio vyakula na matunda yanayoweza kujenga mwili wako kwa haraka

Je, kuna wakati umewahi kujikuta mwili wako hauna nguvu za kutosha kiasi cha kushindwa kupambana na shuruba mbalimbali hata zile za kawaida kabisa? Kama jibu ni ndio basi twende pamoja hapa nikufahamishe matunda na vyakula vitakavyokuokoa katika tatizo hilo.

Ulaji wa ndizi
Ndizi mbivu ni moja ya njia ya kupambana na tatizo hilo kutokana na tunda hilo kuwa na utajiri wa na 'carbohydrates' nyuzinyuzi pamoja na 'fructose' ambavyo kwa pamoja huupatia mwili nguvu na kuupatia stamina.

Juis ya kiazi kikuu,
Juisi hii ni chanzo kizuri cha vitamin A, C ambazo kwa pamoja huujenga mwili kuwa na nguvu za kutosha, lakini pia husaidia kuondoa uchovu.

Mayai
Mayai ni chanzo kizuri cha protini, lakini pia husaidia kupambana na cholesterol ndani ya mwili na hivyo kuusaidia mwili kuwa na nguvu ya kutosha.

Maboga
Maaboga yana vitamin A yakutosha, nyuzinyuzi, lakini pia mbegu zake ni chanzo kizuri cha protin na huongeza madini ya 'magnesium', 'mangenese' na 'zinc' na 'copper'.

Hayo ni machache tu, lakini kwa mengi zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 784 300 300/ +255 769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment