Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 4 July 2016

Je, unazijua faida za kaa kiafya? Zote zipo hapaKAA ni aina ya samaki ambaye ana miguu miwili mikubwa na mingine ikiwa ni midogodogo aarusmbayo mara nyingi kaa huitumia kutembelea akiwa nchi kavu, huku miguu miwili mikubwa ya mbele huitumia kujinda dhidi ya maadui mbalimbali.

Kama ilivyo kwa vitoweo vingine pia kaa naye anafaida zake kiafya ndani ya mwili wa mwadamu.

Miongoni mwa faida za kaa ni pamoja na kulinda afya ya mifupa, ulaji wa kaa huimarisha afya ya mifupa kwasababu ya kuwa na madini ya ‘phosphorus’ na madini ya ‘calcium’ hivyo kwa wale ambao husumbuliwa na matatizo ya maumivu ya mifupa wanashauriwa kutumia kitoweo hiki.

Hulinda afya ya moyo, matumizi ya kaa husaidia kulinda afya ya moyo kwasababu ndani ya kitoweo hicho kuna kirutubisho cha Omega 3 ambayo huhitajika mwilini na husaidia kulinda afya ya moyo, lakini pia husaidia kushusha kiwango cha lehemu yaani ‘cholesterol’ ndani ya mwili. Mbali na hayo pia ulaji wa kaa husaidia kumkinga mhusika dhidi ya kiharusi ‘stroke’

Hupunguza kiwango cha sumu mwilini, kaa husaidia kupunguza kiwango cha sumu ndani ya mwili kwa kuisaidia figo kufanya kazi yake vizuri. Kutokana na kaa kuwa na madini ya ‘phosphorus’ ambayo pia husaidia ufanyaji kazi wa figo vizuri.

Huimarisha mzunguko wa damu ndani ya mwili, faida za kaa husaidia kuimarisha mzunguko wa damu ndani ya mwili.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana  na Tabibu Abdallah Mandai kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment