Monday, 25 July 2016

Kuna faida nyingi za kitunguu swaumu, lakini kikitumika vibaya huweza kuwa na madhara haya


Kama wewe ni mfuatiliaji wa mtandao huu utakuwa ni shahidi kuwa mara nyingi tumekuwa tukieleza faida za kitunguu swaumu katika matibabu.

Lakini leo napenda tuangazie madhara pia ya kitunguu swaumu endapo kitatumika bila kupata ushauri wa wataalam wa masuala ya tiba asili au wajuzi wa tiba zitokanazo na mimea.

Miongoni mwa madhara yanayoweza kusababishwa na kitunguu swaumu ni pamoja na  kusababisha kichefuchefu na wakati mwingine kutapika na kuharisha.

Pia huweza kusababisha hatari ya mhusika kuvuja damu kutokana na kuzuia seli sahani ambazo husaidia damu kuganda. Hivyo kiungo hiki hakishauriwi kutumiwa na kinamama wajawazito au waliotoka kujifungua.

Zingatia
Kutokana na hayo ni vyema ukaepuka kutumia kitunguu swaumu bila kupata ushauri wa wataalam kwani huweza kuwa na madhara kwa afya yako. Kama utakuwa na swali au ushauri unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 784 300 300/ +255 769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment