Saturday, 23 July 2016

Mambo manne utakayoyapata kwenye matunda tu.


Mara kadhaa tumekuwa tukisikia kuhusu umuhimu wa matunda na umuhimu wake ndani ya mwili.

Leo tena ninazo hizi faida nyingine za matunda kiafya karibu tuzifahamu kwa pamoja hapa:-

Matunda mengi yamesheheni nyuzinyuzi (fiber) ambazo kwa pamoja huusaidia mwili kurekebisha mfumo wa umeng'enyaji chakula.

Hupunguza uwezekano wa kukumbwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya moyo, shinikizo la damu na saratani.

Matunda ni miongoni mwa chanzo kizuri cha vitamin na madini ambazo kwa pamoja husaidia mwili kubaki na afya kuwa na nguvu.

Matunda pia huburudisha hivyo yanaumuhimu mkubwa wa kuyatumia mara kwa mara kwani mengi yao huwa na ladha nzuri.

Unaweza kuuliza zaidi kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800 +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment