Wednesday, 27 July 2016

Mbinu 4 za kupambana na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume

Karibuni ndugu wasomaji katika website yetu ya www.dkmandai.com ili tuweze kuendelea kujuzana mambo mbalimbali ya kutujenga kiafya.

Leo napenda tuzungumzie namna ya kupambana na tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume lililochangiwa na tabia ya kujichua (punyeto)

Kwanza acha kabisa kujichua
Kama kweli unapenda kuondokana na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume linalochangiwa na kujichua basi tambua kuwa ni lazima uamue kutoka moyoni kabisa kuacha hiyo tabia. Jisemee moyoni kwamba mimi fulani nimeacha tabia hii na sitarudi nyuma.

Anza kufanya mazoezi
Ikiwa ulikuwa si mtu wakufanya mazoezi itakubidi ubadilike na uanze kufanya mazoezi ili uweze kurudisha nguvu hizo, unahitaji kufanya mazoezi yeyote angalau nusu saa kwa siku. Inaweza kuwa ni mazoezi ya kuruka kamba, kukimbia, kuogele. Mazoezi hayo husaidia mzunguko wa damu kwenda vizuri na hivyo kupunguza tatizo lako la upungufu wa nguvu za kiume.

Pendelea kutumia vyakula vya asili
Ili kupunguza tatizo la upungufu wa nguvu za kiume inabidi ujitahidi kuepuka matumizi ya vyakula vya viwandani ambavyo mara nyingi huwa na kemikali nyingi, huku vikiwa ndio vyakula vinavyoliwa zaidi. Jitahidi kubadilika kwa kuanza kula ugali, karanga, viazi, mihogo na vyakula vyote vinavyoaminika kuwa ni asili.

Pendelea kunywa maji mengi
Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume hutegemea sana mzunguko mzuri wa damu ndani ya mwili ambao huweza kuimarika zaidi endapo mhusika atatumia maji ya kutosha na kufanya mzunguko wa damu kuwa vizuri zaidi.

Kwa amelezo zaidi au ushauri tupigie kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 784 300 300/ +255 769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment