Thursday, 7 July 2016

Pokea hizi faida za kiafya za majani ya mpapai


PAPAI ni tunda ambalo mmea wake hukua hadi kufikia urefu wa mita 30, lakini pia mmea huu unasifika kwa kuwa na uwezo wa kusaidia matatizo mbalimbali kiafya.

Asili ya mpapai ni huko nchini Mexico ingawaje kwa sasa limekuwa ni tunda ambalo hupatikana maeneo mengi duniani.

Uzuri wa mpapai ni kwamba karibu kila sehemu inafaida zake kiafya yaani kuanzia tunda lenyewe, mbegu, majani pamoja na mizizi.

Leo nimeona ni vyema tukazungumzia kuhusu umuhimu wa majani ya mpapai kiafya.

Majani ya mpapai kwanza yamesheheni vitamin B, A, C, D, E pamoja na madini ya ‘calcium’.

Huongeza uimara wa kinga za mwili

Matumizi ya juisi ya majani ya mpapai husaidi kuzuia maambukizi mbalimbali ndani ya mwili

Matumizi ya majani ya mpapai pia husaidia kuzuia malaria

Juisi ya majani ya mpapai ni moja ya msaada kwa wale wenye matatizo ya malaria, licha ya kwamba majani hayo yanauchungu lakini manufaa yake yamekuwa yakionekana ni makubwa zaidi.

Hupunguza maumivu wakati wa hedhi

Majani ya mpapai huweza kutuliza maumivu ya hedhi kwa wanawake, majani hayo huhitajika kuchemshwa ndipo yaweze kuwa msaada kwa tatizo hili.

Zingatia
Ni muhimu kupata ushauri wa wataalam wa tiba asili kabla ya kutumia majani haya kama tiba hivyo unaweza kuuliza zaidi kupitia namba za simu zifuatazo: +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment