Saturday, 9 July 2016

Pokea hizi faida za magimbi katika tiba


Magimbi ni miongoni mwa mazao ambayo hupatikana kwa mfumo wa mizizi. Magimbi hulimwa sehemu mbalimbali hapa nchini hususani maeneo ya mabondeni ambapo maji hupatikana zaidi.

Magimbi yanaelezwa kupatikana zaidi Asia ya Kusini na zao hili limekuwa likistawi zaidi kwenye ukanda wa kitropiki.

Zifuatazo ni baadhi ya faida za magimbi kiafya

Husaidia kupunguza shinikizo la damu.
Magimbi yanauwezo wa kusaidia tatizo hili kutokana na kuwa na madini ya 'potassium' ambayo ni muhimu kiafya ikiwa ni pamoja kusaidia tatizo shinikizo la damu.

Magimbi yamesheheni virutubisho
Magimbi yamesheheni virutubisho na madini mbalimbali ikiwa ni pamoja na madini ya 'calcium', 'copper', 'magnesium', 'manganese'.

Virutubisho vilivyomo ndani ya magimbi ni pamoja na vitamin A, C, nyuzinyuzi 'fiber' pamoja na protin.

Huimarisha kinga za mwili.
Magimbi husaidia kuimarisha kinga za mwili kutokana na kuwa na vitamin C ya kutosha ambayo huimarisha kinga hizo na mwili na kumfanya mhusika kutozongwa na magonjwa ya mara kwa mara.

Hupunguza hatari ya magonjwa ya moyo
Magimbi ni miongoni mwa vyakula ambavyo huingia kwenye orodha ya vyakula ambavyo havina lehemu 'cholesterol'.

Kama ungependa kufahamu umuhimu wa magimbi kiafya unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment