Monday, 11 July 2016

Soma hizi faida 4 za zabibu kiafya ambazo wengi hawazifahamu

ZABIBU ni miongoni mwa matunda yenye virutubisho vingi ikiwa ni pampoja na vitamin A, C,B6 lakini pia ni matunda yenye madini ya potassium, selenium, calcium, phosphorus pamoja na madini ya chuma.

Matunda haya inaelezwa yalianza kulimwa miaka 7,000 iliyopita, lakini kwa hapa kwetu Tanzania zabibu hulimwa zaidi mkoani Dodoma.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) linaeleza kuwa asilimia 71 ya zabibu zote duniani hutumika kutengenezea mvinyo na asilimia 27 pekee huliwa kama matunda ya kawaida, huku asilimia 2 ikifanywa kukaushwa kwa ajili ya matumizi mengine.

Tafiti mbalimbali zinaainisha kuwa zabibu husaidia kuimarisha afya ya akili kutokana na matunda hayo kusaidia mzunguko kwenda vizuri kwenye ubongo.

Miongoni mwa faida za matumizi ya zabibu ni pamoja na kuimarisha kinga za mwili kwa mtumiaji kutokana na kuwa na vitamin C.

Pia zabibu husaidia kupunguza hatari ya mhusika kukumbwa na saratani hususani saratani ya matumbo au matiti.

Aidha, zabibu pia husaidi kupunguza hatari ya matatizo ya figo kutokana na matunda hayo kuwa na uwezo wa kupunguza kiwango cha sumu mbalimbali ndani ya mwili.

Husaidia kurahisisha umeng’enyaji chakula tumboni, hii nayo ni moja ya faida za zabibu kiafya hivyo humsaidia mtumiaji pia kutopatwa na matatizo ya ukosefu wa choo.

Usisite kuwasiliana nasi kwa maelezo zaidi au ushauri tupigie kwa simu namba zifuatazo: +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment