Monday, 25 July 2016

Zifahamu sifa 5 za juisi ya karoti iliyochanganywa na tangawizi


Juisi za matunda ni moja ya kati ya vitu muhimu ambavyo huhitajika katika kujenga afya za miili yetu hususani unapopata juisi za matunda asilia kabisa.

Leo nimeona ni vyema tuzungumzie kuhusu juisi ya karoti iliyochanganywa na tangawizi kiasi.

Juisi hii ya karoti na mchanganyiko wa tangawizi inafaida mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusheheni virutubisho lukuki.

Juisi ya karoti na mchanganyiko wa tangawizi huupatia mwili vitamin A, K, ambazo kwa pamoja husaidia kulinda afya ya kucha pamoja na nywele zetu.

Uwepo wa tangawizi ndani ya juisi hii umekuwa ukiifanya juisi hii kuwa suluhisho la matatizo ya kukatika kwa nywele na kuzifanya kuwa imara zaidi.Hivyo ni juisi nzuri kwa wanawake wanaopenda urembo wa nywele.

Hukinga dhidi ya saratani, matumizi ya juisi ya karoti yenye mchanganyiko wa tangawizi husaidia sana kuukinda mwili dhidi ya matatizo ya saratani za aina mbalimbali kwani husaidia kuua seli zinazoweza kuchangia matatizo ya saratani.

Huimarisha kinga za mwili, juisi hii pia husaidia kuimarisha kinga za mwili kutokana na kuwa na vitamin A ndani yake hivyo kumfanya mhusika kutozongwa na magonjwa ya mara kwa mara.

Hulinda meno na fizi, karoti pekee yake kwanza inatosha kwa kuwa mlinzi mzuri wa kinywa, hivyo matumizi ya glasi moja ya juisi ya karoti iliyochanganywa na tangawizi baada ya kula husaidia sana kulinda afya ya kinywa kwa ujumla.

Kwa sasa naomba kuishia hapo, lakini bado kunamengi kuhusu umuhimu wa juisi hii hivyo kama utahitaji kuyafahamu zaidi unaweza kutupigia kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 784 300 300/ +255 769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment