Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 31 August 2016

Fada 4 za kula samaki mara mbili kwa wiki

Samaki  wanasifika kwa kuwa na virutubisho ambavyo humuongezea mlaji uwezo wa kukumbuka pamoja na virutubisho vyenye uwezo wa kupambana na saratani mwilini.

Hali kadhalika, ulaji wa samaki pia husaidia kuongeza kinga mwilini na kuondoa mafuta mabaya mwilini, hivyo kumsaidia mhusika kuepuka hatari ya kukumbwa na matatizo ya moyo.

Pia matumizi ya samaki huweza kumsaidia mhusika kutokumbwa na matatizo ya mwili kuvimba.

Huweza kupunguza uwezekano wa shinikizo la damu kutokana na kuwa na virutubisho ambavyo husaidia kuboresha afya ya moyo kutokana na kuwa na omega 3 ndani yake.

Aidha, unapotumia samaki husaidia kumpatia mlaji virutubisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na protini, vitamini B3, vitamin D, vitamini B6, Omega 3 Fatty Acids. nk

Pamoja  na hayo, matumizi ya samaki pia husaidia kuongeza uwezo wa kumbukumbu na hivyo kuondokana na tatizo la kusahau sahau.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri zaidi. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment