Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 24 August 2016

Fahamu jinsi hali ya upweke inavyoweza kuharibu afya yako mara moja

Hali ya upweke ni moja ya mambo hatari kwa afya mara. Hali hii mara nyingi huchangiwa na kutengwa na jamii.

Mara nyingi hali hii huweza kuwakumba zaidi wazee wengi ambao kunawakati hujikuta wapweke mara wanapotengwa na familia zao hali inayochangia hata kuwadhoofisha kiafya.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa hali ya upweke huwa na uhusiano wa moja kwa moja na magonjwa kama vile shinikizo la damu, udhaifu wa kinga ya mwili, lakini pia watu hao huwa katika hatari kubwa ya kupata msongo wa mawazo, shambulizi la moyo na kiharusi.

Wazee wengi hukumbwa na hali hii mara baada ya kustaafu kwani wengi wao huwa na mtazamo usio wa kawaida kuhusu kustaafu kazi. Wengi hufikiri kustaafu ni kutengana na marafiki, familia na watu wengine na kutafuta sehemu tulivu za kumalizia maisha kwa furaha. Lakini kumbe kufanya hivyo si jambo jema. Ukweli ni kwamba watu ambao wanaendelea kuwa karibu na wafanyakazi wenzao,familia zao, marafiki na ndugu wengine baada ya kustaafu huzidi kuwa wachangamfu na wasio na upweke. 

Ukweli ni kwamba watu wasio wapweke ni wale walio karibu na familia, marafiki na jamaa.Hivyo unaweza kumuokoa ndugu yako au mzazi wako kutokana na tatizo hili la upweke kwa kuamua kuwa karibu naye kila unapopata nafasi.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri zaidi. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment