Thursday, 4 August 2016

Faida 3 za kiafya zitokanazo na ulaji wa bamia
Bamia ni miongoni mwa mboga za majani ambazo kwa kawaida hulimwa zaidi kwenye maeneo yenye joto, ukanda wa kitropiki ikiwamo mikoa ya Dodoma na Singida.

Pia bamia inafahamika kwa wengi katika jamii kwa ladha yake nzuri inapotumika kama mboga katika baadhi ya milo.

Zifuatazo ni baadhi ya faida za kutumia bamia kiafya:
Bamia ina wingi wa vitamini A ambayo husaidia kuupa mwili kinga ya kupigana na maradhi, lakini kwa wale wenye matatizo ya kuona, kula bamia mara kwa mara husaidia kuimarisha mwanga katika macho yako.

Pia bamia zina wingi wa vitamini K ambayo husaidia kuimarisha mifupa na kuganda kwa damu.

Mbali na hayo, uteute unaopatikana kwenye bamia husaidia kuunda tishu za mwili na ngozi. Hivyo kusaidia husaidia kujenga ngozi.

Tunatoa ushauri zaidi juu ya lishe bora na mapngilio wa mlo tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment