Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 20 August 2016

Faida 4 za kiafya za kula polepoleWatu wengi saizi wamekuwa na pilikapilika nyingi za kujipatia kipato  ambazo kuna wakati huwa zinavuruga kabisa hata mpango wa mlo wetu.

Kuna baadhi ya watu hujikuta hawatulii mezani kabisa wakati wa kula kwasababu ya kuwa na harakati za kukimbizana na maisha.

Leo napenda tufahamishane huu umuhimu wa kula taratibu na faida zake kiafya:-

1. Ulaji wa utulivu na polepole husaidia kuboresha umen'genyaji wa chakula tumboni, hii inamaana kwamba siku zote umeng'enyaji wa chakula huanzia mdomoni hivyo ni muhimu kutafuna taratibu na vizuri chakula ili kurahisisha umeng'enyaji wa chakula kinapofika tumboni.

2. Ulaji wa polepole husaidia kupunguza mawazo 'stress'

3. Ulaji wa polepole husaidia kufurahia chakula na kusikia vizuri 'taste' ya chakula.

4. Husaidia kupunguza uzito, tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa ulaji wa polepole husaidia sana mhusika kuwa na uzito mkubwa. Mara nyingi mtu anayekula haraka hujikuta amakula chakula kingi kwa mda mfupi hivyo kama alikuwa anahitaji kuwa na uzito unaokubalika kiafya hujikuta anashindwa.

Unaweza kututembelea ofisi za WUTA zilizopo, Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam ili kupata ushauri zaidi kuhusu lishe mbalimbali na namna ya kuziandaa. Au tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment