Monday, 15 August 2016

Faida 5 muhimu utakazopata ukitumia fursana leo


Fursana ni moja ya tunda ambalo lina virutubisho vingi ambavyo vinapotumika vizuri huweza kuwa na manufaa kiafya.

Miongoni mwa faida za tunda hili ni pamoja na kurekebisha kiwango cha sukari ndani ya mwili pamoja na kupunguza kiwango cha cholesterol ndani ya mwili.

Pia ndani ya fursana kuna vitamin C ambayo husaidia mwili kulinda dhidi ya magonjwa mbalimbali, lakini pia ndani yake kuna vitamin K ambayo hulinda afya ya mifupa.

Ndani ya fursana pia kuna madini ya copper, zinc, magnesium pamoja na madini ya chuma ambayo husaidi kuongeza damu mwilini.

Madini mengine yanayopatikana ndani ya matunda haya ni pamoja na manganese selenium ambayo huwa na mchango mkubwa ndani ya mwili pia.

Zifuatazo ni faida za fursana mwilini
1. Huamsha afya ya akili.
2.Huboresha afya ya mifupa.
3. Husaidia kurekebisha uzito wa mwili.
4.Ni matunda mazuri kwa afya ya moyo.
5. Hupunguza uwezekano wa kukumbwa na saratani.

Unaweza kututembelea ofisi za WUTA zilizopo, Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam ili kupata ushauri zaidi kuhusu lishe mbalimbali na namna ya kuziandaa. Au tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment