Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 26 August 2016

Fanya yafuatayo ili kuwa na afya ya bora

Huenda kila siku umekuwa ukijihisi mchovu na kushindwa hata kufanya shughuli zako za kila siku na umekosa majibu ya moja kwa moja ya kutambua chanzo cha tatizo hilo.

Sasa hapa napenda ufahamu haya machache ya kufanya ili ubaki kuwa na afya bora pamoja na kuwa mchangamfu.

Jitahidi kunywa kiasi cha kutosha cha maji safi na salama, unywaji wa maji utasaidia mwili kurudisha maji na madini yaliyopotea mwilini. Maji ni muhimu katika ufanyaji kazi wa mifumo mbalimbali ya mwili.

Jifunze kufanya mazoezi ya kunyosha viungo vya mwili unapoamka, hii husaidia kuboresha
mzunguko wa damu na kukusaidia kuondoa maumivu ya viungo.

Kamwe usianze siku yako bila kifungua kinywa. Tafiti zinaonyesha kuwa, kifungua kinywa ni muhimu kwa afya zetu.

Usitumie vyakula vyenye wanga kabla ya saa moja kupita baada ya mazoezi. Hii itaulazimisha mwili wako kuanza kutumia kiasi cha mafuta yaliyohifadhiwa mwilini badala ya kutumia chakula ulichokula. Unaweza kula matunda katika muda huo 

Pata muda wa kutosha wa kupumzika pamoja na kulala mara baada ya shughuli zako za kila siku.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri zaidi. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment