Friday, 12 August 2016

Haya ndio matunda mawili yenye uwezo wa kupunguza maumivu ya viungo
Maumivu ya mishipa au gout yanaweza kuleta maumivu makubwa katika maungio hasa katika kidole gumba cha mguu.

Lakini pia unaweza pia kujisikia maumivu katika kifundo cha mguu, magotini au katika maungio mengine ya mwili.

Kitu kikubwa kinachosababisha maumivu hayo ni kiasi kingi cha asidi katika mzunguko wa damu. 

Ikiwa unasikia maumivu kila mara katika mikono, vidole, magoti, katika maungio mbalimbali mwilini unashauriwa ukapate vipimo zaidi.

Yafuatayo ni baadhi ya matunda ambayo huweza kupunguza tatizo hilo:-

1. Nanasi

Nanasi lina kimeng’enya mhimu kiitwacho ‘bromelain’ ambacho kina sifa ya kuzuia muwako wa ndani ya mwili (inflammation). Kwahiyo mhusika wa tatizo hili anapotumia tunda  kila siku  huweza kusaidia  kupunguza maumivu yatokanayo na gout.

.
2. Zabibu

Zabibu zina kiasi kingi cha kiuaji sumu na zinaweza kupunguza maumivu ya gout  kwa haraka zaidi. Mbegu za tunda la zabibu zina kitu mhimu kiitwacho  phenomenology ambacho ni kiuaji sumu kingine kinachosaidia kupigana na aina zote za maumivu ya mishipa ikiwemo gout. Hivyo unashauriwa kutumia tunda hili mara kwa mara ili kuepuka tatizo hili.

Ushauri huu umetolewa na shirika liliso lakiserikali liitwalo The Work Up Tanzania (WUTA) unaweza kuwasiliana nao zaidi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com
No comments:

Post a Comment