Tuesday, 9 August 2016

Hivi ndio vyakula vyenye uwezo wa kuongeza kinga za mwili


Mara nyingi tumekuwa tukipokea maswali kuhusu maana ya kinga ya mwili wengi wakihitaji kujua kinga hizo ni kitu gani na je ni hufanyika ilikuziimarisha.

Kimsingi kinga za mwili huweza kupanda au kushuka kutokana na chakula unachokula au vinywaji unavyokunywa.

Mwili ulibuniwa na Mungu uweze kujitibu wenyewe bila kuhitaji dawa yoyote isipokuwa mwili unaweza kupambana na matatizo kutokana na vyakula unavyokula na kunywa. Shida ni kuwa watu wengi hatujuwi tule nini kwa ajili ya nini, mara nyingi tunakula ili tushibe.

Fanya chakula kiwe ndiyo dawa zako na si dawa kuwa chakula kwako. Kinga yako inapokuwa na nguvu  ya kutosha huwezi kuugua ugonjwa wowote kirahisirahisi.

Vifuatavyo ni vyakula 14 vinavyoweza kukusaidia kuongeza kinga za mwili.

Matunda 

Katika mlo wako wowote jitahidi usiache kujumuisha angalau tunda la aina moja. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, mtu asiyekula matunda ana hatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa zaidi ya mlaji wa matunda.

Asali
Asali halisi husaidia kuimarisha pia kinga za mwili, lamba kijiko kimoja cha chakula kila siku kutwa mara tatu kwa mwezi mmoja itasaidia kuimarishakinga zako za mwili.

Ubuyu
Pata kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu  kila siku kwani juisi hiyo inawingi wa vitami C nyingi ambazo husaidia pia kuimarisha kinga za mwili.

Nazi

Matumizi ya nazi huweza kusaidia kuimarisha kinga za mwili kutokana na kuwa na mafuta yaitwayo ‘medium chain fatty acids’ ambayo husaidia kuimarisha kinga ya mwili na hivyo kuupa mwili uwezo wa kuyashinda maradhi mbalimbali.

Tangawizi.
Ni moja ya kiungo ambacho kinaingia kwenye orodha hii ya kuimarisha kinga za mwili pia.

Kwa mengine mengi zaidi unaweza kutupigia kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com Au fika ofisi zetu za The Work Up Tanzania (WUTA) zilizopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment