Saturday, 13 August 2016

Hivi ndivyo tangawizi inavyoweza kuzuia tatizo la kukatika kwa nywele


Mara kadhaa tumeshazungumza kuhusu faida za kiungo cha tangawizi ni kweli ni moja ya kiungo chenye faida mbalimbali.

Miongoni mwa faida za kiungo hicho ni pamoja na kupunguza maumivu ya viungo, kurekebisha mmeng'enyo wa chakula tumboni pamoja na kusaidia kulinda afya ya figo na mengine mengi.

Hapa leo napenda kuzungumzia namna tangawizi inavyoweza kupunguza tatizo la kukatika kwa nywele kwa kinadada.

Matumizi ya tangawizi husaidia kuzifanya nywele kuwa na afya na hivyo kuzifanya kutokatika ovyo wakati wa kuzichana au kusukwa, pia kiungo hicho husaidia kulinda nywele dhidi ya mba.

Ikiwa utapenda kufahamu namna ya kutumia kiungo hiki kwa uzuri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/+255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kwamba ushauri huu umeletwa kwako chini ya Shirika lisilokuwa la kiserikali la THE WORK UP TANZANIA (WUTA). Shirika ambalo linamalengo ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii matumizi ya lishe bora pamoja na rasilimali zinazotuzunguka katika jamii.

No comments:

Post a Comment