Monday, 1 August 2016

Hivi ndivyo vyakula vitakavyokupa lishe bora mwilini mwako


Ili kuielimisha jamii juu ya magonjwa na matatizo mbalimbali ya kiafya, bado tunaendelea kuwaletea makala mbalimbali kwa msaada wa shirika lisilolakiserikali la THE WORK UP TANZANIA (WUTA) ambalo limelenga kuikwamua jamii dhidi ya umasikini, ujinga na maradhi kupitia vitu vinavyotuzunguka kila siku.

Vyakula vya kujenga mwili au protini
Protini ni chakula cha kujenga mwili na ni cha lazima kwa kumfanya mtu akue vizuri kwa misuli na sehemu zingine nyingi za mwili ziwe na afya. Ili kukua na kuwa na nguvu kila mtu lazima ale protini za kutosha kila siku.

Vyakula vyenye protini kwa wingi ni nyama, maziwa, kuku, jibini, mayai, maharagwe ya soya, Samaki, wadudu, vyakula vya maji ya baharini.

Vyakula vyenye protini kidogo ni maharagwe, karanga, mboga za majani, dengu, nafaka (ngano, shayiri, kokwa (nuts) mtama n.k.

Vyakula vya kutia nguvu mwilini 
Vyakula vya sukari na vya wanga hutia nguvu mwilini. Kwa jinsi mtu anavyofanya kazi kwa nguvu ndivyo anavyohitaji nguvu zaidi lakini kula vyakula hivi peke yake bila protini hufanya miili yetu idhoofike.

Vyakula vya wanga nafaka, (ngano, mpunga, mahindi, shayiri, mtama, ulezi) viazi mviringo, viazi vitamu viazi vikuu mihogo ndizi za kupika, magimbi.

Vyakula vya sukari ni:- matunda, sukari ndizi mbivu, asali, maziwa.

Vyakula vya kuweka akiba mwilini mafuta
Mafuta ni aina nzito ya akiba ya nguvu mwilini. Miili yetu huyabadilisha mafuta kuwa sukari. Wakati nguvu zinapohitajika kula mafuta mengi kunawezesha kumdhuru mtu, lakini mafuta ya kiasi katika mlo huleta afya bora.

Miili yetu ni rahisi kuzongwa na magonjwa ikiwa wahusika hawatakula vyakula vyenye vitamin zinazohitajiwa.

Kwa maelezo zaidi na ushauri unaweza kutupigia simu kwa namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment