Thursday, 25 August 2016

Hizi hapa njia za kumaliza tatizo la kuwahi kufika kileleni mapema


Kitendo cha kuwahi kufika kileleni au kuwahi kumaliza tendo la ndoa ni hali ambayo inampata mwanamme ambapo hutoa manii kabla ya kuanza tendo la ndoa au muda mfupi tu baada ya kuanza tendo.

Mara nyingi wanaume wenye tatizo hili hutoa mbegu hata baada ya maandalizi kidogo sana. Tatizo hili hujidhihirisha zaidi kwa vijana wenye umri mdogo.

Hata hivyo, tatizo hili huweza kumkumba kila mwanaume katika maisha yake, lakini shida huja pale tatizo hili linapokuwa la kudumu. 

Hakuna chanzo cha moja kwa moja cha tatizo hili, lakini moja ya sababu ambayo imekuwa ikitajwa sana ni pamoja na hali ya wasiwasi pamoja na mishipa ya fahamu inahusika sana na tatizo hili. Hali hiyo inaweza kutokea iwapo unapompata mpenzi mpya au endapo mwanaume husika atakuwa hajafanya  tendo hilo kwa kippindi  kirefu.

Njia zifuatazo huweza kukusaidia kuondokana na tatizo hilo:-
Kwanza unapokuwa ukishiriki tendo jitahidi kufanya taratibu usiwe na papara, Wengi wamejikuta wakiwa na shida hii kutokana na kuwa na papara au haraka katikati ya tendo hilo. Ukweli ni kwamba unapofanya taratibu ni njia nzuri zaidi kwani utamfikisha mwenzi wako na wewe utachelewa kufika kilele pia. 

Kuwa mtundu, hapa namaanisha kuwa ni lazima uwe mjanja katika suala hili ikiwemo suala la kubadilisha 'style'. Asilimia kubwa hupenda kutumia 'style' ya mwanamke kuwa chini mwanaume juu style ambayo huleta msuguano mkubwa kwenye kichwa cha uume na kumsababishia mwanaume kuwahi zaidi kufika kileleni, hivyo ni vyema ukabadili 'style' mara kwa mara.

Unapokuwa katika tendo hakikisha unaondoa mawazo yote ya kuwa unafanya ngono na badala yake unaweza kuwaza au kufikiria kuhusu maisha kidogo au masuala yako ya kikazi wakati unaendelea na tendo hii itakupunguzia hisia kali za mapenzi na kuchelewa kufika.

Unapoona unakaribia kutoa mbegu basi unaweza kusimama angalau kwa sekundi 30 kisha unaanza upya. Hii husaidia sana kuchelewa kufika kileleni na hauta weza kumaliza kwa haraka.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri zaidi. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment