Wednesday, 31 August 2016

Hizi ndio sababu ambazo zinakufanya uchelewa kuona siku zako na huna mimba


Kuna baadhi ya wanawake wamekuwa wakikosa la kufanya pale wanapoona siku zao za mzunguko (hedhi) zimefika halafu bado hawajaona siku hizo.

Hali hiyo huwapelekea wengi wao kuwa na maswali mengi, huku wengi wao wakianza kufikiri kuhusu ujauzito.

Sasa leo napenda tufahamishane hizi sababu ambazo huweza kuchangia siku zako kuchelewa kuonekana:-

1. Mabadiliko ya shughuli zako za kila siku
Huenda umeajiri sehemu mpya ambayo inakulazimu kubadili mfumo wako mzima wa maisha ya kila siku ikiwa ni pamoja na muda wa kuamka au umesafiri kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, hali hiyo na mengine huweza kuwa chanzo cha mabadiliko ya mzunguko wako ikiwa ni pamoja na kuchelewa.

2. Msongo wa mawazo 'stress'
Msongo wa mawazo ni mojawapo ya sababu ambazo huweza kuchangia kuvuruga mzunguko wako wa hedhi na kuchangia siku zako kuchelewa pia.

3. Ugonjwa
Pale mwili unapopatwa na mabadiliko yakiwemo ya kuumwa nayo huweza kuwa sababu ya kubadili mzunguko wako wa hedhi na kuchangia pia kuchelewa kuona siku zako, kwahiyo ukiona hali hiyo unaweza kurudisha nyuma kumbukumbu zako na kukumbuka endapo wiki moja au mbili nyuma kama ulikuwa unaumwa au ulikuwa sawa.

4. Masuala ya uzito.
Kuongezeka au kupungua kwa uzito huweza pia kuwa chanzo cha tatizo hili, hii ni kwasababu watu wenye uzito mkubwa au wenye uzito mdogo kunawakati huweza kujikuta wakiingia kwenye tatizo kama hili la kuchelewa kuona siku.

Unaweza kuwaona wataalam endapo utakuwa na tatizo hili ili kupata ushauri zaidi

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri zaidi. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment