Tuesday, 2 August 2016

Je, unafahamu faida za kufanya mazoezi kabla ya kunywa chai? zipo hapa


Siku zote tumekuwa tukihimizana kuhusu kufanya mazoezi mara kwa mara kutokana na kuwa na umuhimu mkubwa kwa afya zetu.

Hata kama unapata lishe bora, lakini huna mazoezi basi usitarajie kama utabaki kuwa na afya bora

Leo apenda kuzungumzia umuhimu wa kufanya mazoezi kabla ya kufungua kinywa.

Mazoezi ni muhimu sana kwani hupunguza mafuta ya ziada mwilini na kwa mujibu wa utafiti wa Dk Jason na Nor Farah (2004) wa Chuo Kikuu cha Glasgow, Scotlanda unasema kwamba unapofanya mazoezi kabla ya kufungua kinywa wakati tumbo likiwa tupu, ni bora zaidi kuliko unapofanya mazoezi baada ya mlo wowote.

Mazoezi yanapoambatana na lishe bora ni muhimu sana kwa afya kwani huzuia magonjwa sugu kama kisukari, magonjwa ya moyo, saratani pamoja na shinikizo la damu.

Aidha, unapojenga utaratibu wa kufanya mazoezi basi huwa ni nafasi nzuri sana ya kujiongezea kipato kwani humfanya mhusika kuwa na afya bora ambayo humsaidia kuwa na uwezo mzuri wa kufanya kazi kwa muda mrefu.

Faida nyingine ya kufanya mazoezi mara kwa mara, kabla ya mlo ambazo hazionekani ikiwa ni pamoja na kujiimarisha kiakili, ambapo matokeo yake ni kuwa na furaha , hii ni kutokana na kuzalishwa kwa wingi aina ya kemikali iitwayo 'endorphins'

Kutokana na umuhimu wa mazoezi ni vyema kuchukua muda wako hata kidogo tu kwa kuanza kufanya mazoezi kwani utajisikia vizuri na kuwa mwenye afya. Anza kufanya mazoezi angalau kwa muda wa robo saa asubuhi kabla ya kunywa chai.

Kwa maelezo na ushauri zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment