Friday, 5 August 2016

Je, unajua vyakula gani hutengeneza mlo kamili kwenye miili yetu? vyote vipo hapa soma

Huenda mara nyingi umekuwa ukisikia kuhusu umuhimu wa kupata mlo kamili? lakini labda haufahamu mlo kamili huo unakuaje.

Hapa ninayo orodha ya vyakula ambavyo kwa pamoja hufanya majumuisho ya mlo kamili kama ifuatavyo:-

Mlo kamili unatokana na kula angalau aina moja ya chakula kutoka kwenye kila moja ya makundi haya ya chakula yaani nafaka, ndizi za kupika, mizizi na kiazi, jamii ya kunde, njugu na vyakula vyenye asili ya wanyama, mboga, matunda, mafuta kiasi na sukari.

Zingatia:- Maji hayahesabiwi kuwa ni chakula, lakini ni sehemu muhimu ya chakula.

Kama unahitaji ushauri zaidi kuhusu uandaaji wa vyakula vyenye lishe bora unaweza kututafuta 'The Work Up Tanzania' (WUTA) tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandait@gmail.com

No comments:

Post a Comment