Saturday, 6 August 2016

Lishe bora hutegemeana na maandalizi sahihi,fahamu hapa namna ya kuandaa lishe


Tumekuwa tukizungumza mara kadhaa sasa kuhusu umuhimu wa lishe bora, lakini ni vyema ikafahamika lishe bora haiwezi kuwa bora endapo maandalizi yake yatakuwa hayazingatii kanuni za kiafya.

Leo Shirika la THE WORK UP TANZANIA (WUTA) kupitia mtaalam wetu Tabibu Mandai anatueleza jinsi ya kuandaa chakula kwa kufuata taratibu za kiafya.

1. Kwanza nawa mikono yako kabla ya kukamata chakula au kuandaa chakula.

2. Pika vizuri bidhaa za nyama kabla ya kula. Osha vizuri vyombo na vifaa vyote vinavyotumika kutayarisha nyama, vyakula vya baharini, mayai ili vijidudu kutoka kwenye vyakula hivyo ambavyo havijapikwa visienee kwenye chakula ambacho tayari kimepikwa au vyakula vingine ambavyo huliwa bila kupikwa.

3. Osha au menya matunda na mbogamboga, au pika kabla ya kutumia. Hii huua vijidudu vya magonjwa kutoka udongoni mahali vinapolimwa, na vijidudu vingine ambao huingia wakati wa usafirishaji au kuhifadhi.

4. Kula chakula moja kwa moja baada ya kupikwa, au hifadhi chakula kilichopikwa kwa kufunika vizuri sehemu salama ili kisifikiwe na nzi na uchafu hadi kitakapoliwa.

5. Hifadhi chakula kwa njia ambayo huhakikisha usalama wake dhidi ya wadudu na wanyama wadogo ambao wanaweza kueneza vijidudu vya magonjwa.

6. Tunza eneo la kupikia katika hali ya usafi. Osha vyombo vya kupikia na kulia, sehemu za kukatia, na vifaa kila mara baada ya kutumia na uruhusu kukauka vizuri.

7. Chakula kihifadhiwe kwenye hali ya ubaridi, ili kusaidia kisiharibike haraka.

Unaweza kupata ushauri kutoka kwetu tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment