Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 23 August 2016

Mambo 5 muhimu ya kuzingatia wakati wa kula na watoto


Kwanza ni vyema ikafahamika kuwa wakati wa kula ndio muda mzuri wa familia kukutana pamoja na kufurahia wakati huo.

Kuna mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kula kama ifuatavyo:-

Tayarisha chakula vizuri katika mazingira ya usafi kisha mle pamoja kama familia wakiwemo watoto.

Kama ikibidi unaweza kutowaruhusu watoto kula huku wakiangalia runinga au kucheza wakati wa kulakwani huweza kuchangia watoto kutokula vizuri.

Epuka kutumia wakati wa kula kumsema mtoto, kwani huweza kumfanya mtoto kushindwa kula vizuri au kususa kula.

Tambua kuwa hali ya kula kwa pamoja hutia nguvu familia na kuiunganisha pamoja na kuwajengea watoto tabia ya kula vizuri.

Ni vyema ikafahamika kuwa kitendo cha watoto kula pamoja husaidia kujenga mshikamano ndani ya wanafamilia, lakini hujenga mahusiano mazuri pia ndani ya wanajamii.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri zaidi. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment