Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Sunday, 21 August 2016

Mambo matano yanayochangia hali ya uchovu kila siku


Je, unaaumbuliwa na uchovu muda wote? kama jibu ni ndio naomba kwa pamoja tufahamishane hizi sababu chache ambazo zimekuwa zikichangia tatizo hilo.

Zifuatazo ni sababu ambazo huweza kuchangia hali ya uchovu kwako kila siku.

Kuishi bila kufanya mazoezi
Inawezekana umekuwa ukiishi bila kufanya mazoezi huenda kila siku ukiamka unajiandaa na kuelekea eneo lako la kazi pasipo kufanya japo aina nyepesi ya mazoezi hilo nalo tambua ni tatizo na huweza kuchangia kuzongwa na hali ya uchovu kwako kila siku.Tambua kuwa mazoezi ni muhimu kwa afya zetu.

Msongo wa mawazo stress.
Unapokuwa na msongo wa mawazo kuna nafasi kubwa ya kusumbuliwa na hali ya uchovu wa mara kwa mara hivyo ni vyema kupunguza mawazo ili kuepuka tatizo hili.

Kutokunywa maji ya kutosha.
Hii nayo ni moja ya sababu ya hali ya uchovu, wengi wetu tumekuwa si wanywaji sana wa maji ya kunywa hali ambayo hushindwa kuupa nafasi mwili kufanya shughuli zake ipasavyo na kuchangia mwili kuhisi hali ya uchovu. Wataalam wa masuala ya afya wanashauri kunywa angalau glasi 8 za maji kila siku ili kuufanya mwili kuwa katika hali nzuri.

Kukosa muda wa kutosha wa kulala
Wataalam wanashauri kulala angalau saa 8 kila siku ili kuendela kuwa na afya njema na kuwa mchangafu, lakini pia katika hili lazima uzingatie mazingira yako ya kulala kama ni rafiki kwako na hayana kelele amabyo yatakuruhusu kulala vizuri.

Tabia ya kula vitu vitamu 
Ulaji wa vyakula vitamu nao unaelezwa kuchangia hali ya uchovu, hivyo ni vyema kuepuka matumizi ya vyakula vya aina hiyo kwa muda mrefu au kupita kiasi.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambali linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi. Unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri zaidi. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.
No comments:

Post a Comment