Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 20 August 2016

Mambo muhimu ya kuyafahamu kuhusu tunda la fenesi


Fenesi kama ilivyo kwa matunda mengine nalo limesheheni virutubisho mbalimbali ambavyo ni pamoja na wanga, protini na nyuzinyuzi.

Wengi wamekuwa wakitumia tunda hili bila kufahamu kuwa  ulaju wa tunda hili unapata vitamin C ambayo husaidia kuimarisha mfumo mzima wa kinga ndani ya mwili.

Tunda hili linaelezwa kuwa na uwezo kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya saratani na kuondoa sumu mwilini pamoja na kuimarisha uwezo wa kuona na kuimarisha mifupa.

Kutokana na kuwa na vitamin C basi hulifanya tunda hili kumsaidia mlaji kutopata magonjwa ya kifua na mafua mara kwa mara.

Ulaji wa tunda hili husaidia kuongeza nguvu mwilini kutokana na kuwa na wanga .

Hivyo basi, kutokana na faida hizo Shirika la WUTA linawashauri watu kuanza kupendelea matumizi ya tunda hili mara kwa mara.

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana na wataalam wa Shirika la WUTA kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment