Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 20 August 2016

Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa ujauzito


Siku zote afya bora ya mtoto huanza kujengwa tangu mtoto anapokuwa tumboni mwa mama, hivyo mama anayo nafasi kubwa ya kuhakikisha mtoto anazaliwa akiwa ana afya njema.

Hapa ninayo mambo muhimu ya kuzingatia kwa mama ambaye ni mjamzito:-

Hakikisha unahudhuria kliniki wakati wote wa ujauzito ili kutambua hali ya mtoto wako.

Mama mjamzito anapaswa kula vizuri, kwani chakula anachokula mama ndiyo hicho pia ambacho mtoto hupata virutubisho muhimu kupitia chakula hicho. Pia ni vyema kuhakikisha kila siku mama anapata chakula cha kutosha pamoja na matunda.

Pia mama mjamzito anapaswa kuzingatia vinywaji vya kutumia wakati wa kipindi hiki, ikumbukwe kuwa mama anapokuwa katika hali ya ujauzito hapaswi kutumia aina yoyote ya kilevi .

Mazoezi mepesi ni muhimu wakati wa kipindi hiki, lakini ni vizuri kupata ushauri wa aina ya mazoezi yanayofaa wakati wa ujauzito na kuzingatia muda wa ujauzito.

Kuacha uvutaji wa sigara, matumizi ya sigara wakati wa ujauzito huwa na madhara kwa mtoto tumboni, huweza kusababisha utokaji wa mimba pia.

Mama mjamzito anahitaji kupata muda wa kutosha wa kulala

Unaweza kututembelea ofisi za WUTA zilizopo, Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam ili kupata ushauri zaidi kuhusu lishe mbalimbali na namna ya kuziandaa. Au tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment