Tuesday, 16 August 2016

Mbinu 2 muhimu za kuchagua matunda mazuri yenye virutubisho


Matunda ni moja ya vitu muhimu sana katika miili yetu kutokana na kuwa na virutubisho mbalimbali ambavyo vinahitajika sana ndani ya mwili.

Hata hivyo, ili kuvipata virutubisho hivyo muhimu kupitia matunda ni lazima muhusika apate matunda ambayo yapo fresh yaani mazuri.

Miongoni mwa mambo ya kuzingatia ili kupata matunda fresh ni pamoja na hizi zifutazo:-

Hakikisha unakula matunda ya msimu.
Wakati unapokwenda sokoni au gengeni kuchangua matunda ni vyema kuzingatia matunda unayochagua yawe ni ya msimu huo, kwani yasipokuwa yamsimu huo basi tambua kuwa utakuwa na nafasi ndogo ya kupata kwanza matunda ya kutosha kwa sababu gharama yake itakuwa juu, lakini pia kupata matunda yasiyokuwa bora kwani huweza kuwa yamelazimishwa kuiva kwa kuvundikwa.

Yaguse matunda wakati wa ununuzi
Ili kutambua ubora w tunda unalohitaji kununua ni vyema kuligusa kwa mkono wako mwenyewe ili kugundua ubora wa tunda husika. Tatizo ni kwamba wengi wanapokwenda sokoni kununua matunda huwaachia wauzaji kazi ya kuchagua na matokeo yake hujikuta wakiwekewa matunda yasiyo bora au yaliyoanza kuharibika.

Unaweza kututembelea ofisi za WUTA zilizopo, Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam ili kupata ushauri zaidi kuhusu lishe mbalimbali na namna ya kuziandaa. Au tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment