Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 5 August 2016

Mbinu 5 za kula chakula chenye lishe bora, hata kama unauwezo mdogo wa kiuchumi

Familia ikipata chakula (Picha kwa msaada wa mtandao)
Hivi unafahamu kuwa pamoja na kuwa na hali yako duni ya kimaisha au kipato, lakini bano unaweza kuwa na nafasi nzuri ya kula vyakula vyenye lishe bora

Hapa leo napenda kukupatia mbinu zitakazokufanya upate lishe bora pamoja na kuwa na hali duni ya kiuchumi.

Mbinu za kupata mlo wa kutosha na wenye lishe bora
1. Nunua vyakula vya kawaida visivyo ghali kama vile maharagwe, nafaka. vyakula hivi vina virutubishi zaidi na gharama yake ni nafuu kuliko vyakula ambavyo vimetengenezewa viwandani kama vile mikate mweupe, biskuti, na supu za kwenye makopo.

2. Kama unaishi mazingira yanayokuwezesha kulima angalau bustani jitahidi ufanye hivyo na upande mbogamboga za majani ambazo nazo ni muhimu kwa afya na si gharama kuzihudumia

3. Pia unaweza kufanya ufugaji wa kuku ili kupata mayai na nyama au kufuga samaki pia, vitoweo hivyo vyote vitaisaidia familia yako kupata mahitaji ya lishe bora kila siku ndani ya mwili wako.

4. Jifunze kujenga utaratibu wa kununua chakula kwa wingi. Unaponunua chakula kidogo kidogo huweza kuwa gharama kuliko unaponunua kwa wingi .

5. Epuka vyakula vya makopo yakiwemo maziwa yaliyoongezewa ladha ambavyo huuzwa kwa ajili ya watoto wachanga na watoto wadogo. Matumizi ya vyakula hivyo ni sawa na kupoteza fedha kwani maziwa ya kawaida ya wanyama, au vyakula ambavyo vimepikwa vizuri na kupondwapondwa vina gharama nafuu zaidi na pia huleta afya zaidi kwa watoto.

Acha kutumia fedha zako kwenye mambo ya anasa na badala yake anaza kutumia fedha kidogo unayoipata kwa ajili ya chakula. Kumbuka kuwa sigara, pombe au soda hugharimu fedha nyingi na havina faida yoyote kilishe.

Unaweza kupata ushauri wa masuala mbalimbali kuhusu lishe bora kupitia Shirika la THE WORK UP TANZANIA (WUTA) kutoka kwa Tabibu Mandai mpigie kwa namba za simu zifuatazo 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment