Monday, 15 August 2016

Mengine mazuri yakuyafahamu kuhusu mafuta ya mdalasini

Mdalasini ni moja ya kiungo ambacho kinamama hukitumia sana kwa malengo yakuongeza ladha kwenye chai.

Lakini kiungo hiki pia nacho hakiishii kuleta ladha nzuri tu kwenye chai bali pia ni mojawapo ya kinga na tiba ya magonjwa mbalimbali.

Unapopata mafuta yatokanayo na huu mdalasini basi husaidia sana kuondosha shida ya fangasi hususani aina ya 'candida'

Matatizo ya maumivu ya viungo nayo huweza kupata ufumbuzi kwa kutumia mdalasini hii ni kwa sababu kiungo hiki kinautajiri mkubwa wa madini ya magnesium ambayo pia uimarisha afya ya mifupa. Pia huweza kutumia mafuta yake kwa kuchua sehemu za mwili.

Unaweza kututembelea ofisi za WUTA zilizopo, Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam ili kupata ushauri zaidi kuhusu lishe mbalimbali na namna ya kuziandaa. Au tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment