Sunday, 28 August 2016

Namna ya kufanikiwa kimaisha kwakutumia mawazo binafsi


Kuna watu wamezoea kufanya baadhi ya mambo mara baada ya kuhamasishwa na watu fulani fulani ambao huwazunguka katika maisha yao ya kila siku, lakini je, umewahi kujiuliza itakuaje kesho waatu hao ikiwa hawatakuwa karibu na wewe?

Basi hapa leo napenda kukufahamisha mbinu za kujihamasisha wewe mwenyewe binafsi bila kutegemea watu wengine na ukaweza kufanikiwa.

1. Anza kwa kutazama yalea mambo makubwa uliyowahi kuyafanya.
Hii ni mbinu nzuri ya kukusaidia kujihamasisha wewe mwenyewe, angalia umewahi kufanya mambo mangapi makubwa na uliyafanikisha, kumbuka namna ulivyofanikisha kuwashawishi watu fulani kukuamini juu ya jambo lako na ukafanikiwa kuaminika. Hayo na mengine mengi yanaweza kukujengea na kukufanya ukafanikiwa zaidi.

2. Usiache kujifunza kila siku.
Soma vitabu, makala mbalimbali pamoja na magazeti kwani hii nayo ni mbinu nzuri ya kukufanya ukabaki kwenye hali nzuri na hamasa kubwa ya kufanikiwa katika kile kitu unachokipenda.

3. Punguza maneno zaidi kuwa mtu wa vitendo
Acha kuwa muongeaji sana, bali kuwa mtu wa kutekeleza mambo uliyojipangia ili kufikia malengo yako. Kumbuka kuwa siku zote watu hawaangalii maneno bali zaidi watahitaji kuona ulichofanya. Tabia hii itakupa uwezo na ujasiri wa kusonga mbele zaidi.

4. Usiwe mtu wa kurukaruka simamia jambo moja
Watu wengi wenye kufanya kila kitu huwa mwisho wa siku wanaishia kushindwa, na kukata tamaa ya kuendelea kufanya hata mambo mazuri yaliyokuwa na manufaa kwao. Jifunze kuchagua jambo moja unaloweza kulifany na hakikisha unakwenda nalo hadi mwisho kwani kwa kufanya hivyo kutakufanya kufanya mambo yako kwa umakini mkubwa na mafanikio.

5. Punguza kulalamika 
Kulalamika hakunafaida yote kwako na hata unapolalamika hakubadilishi maisha yako tambua kuwa kulalamika hupoteza malengo yako na hata heshima yako pia na kukufanya ushindwe kusonga mbele.

6. Kuwa karibu na wale wenye mawazo chanya.
Tembea na uwe miongoni mwa watu chanya wenye kutamamani kufikia mafanikio makubwa ya kutimiza na kufikia ndoto zao maishani. 

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri zaidi. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.


No comments:

Post a Comment