Monday, 29 August 2016

Nyanya na umuhimu wake kiafya


Nyanya ni moja ya kiungo ambacho hutumika karibu kila siku katika familia zetu hususani katika kusaidia kuandaa vyakula mbalimbali hususani mboga.

Lakini mbali na matumizi hayo nyanya pia inafaida zaidi ya kutumika kama kiungo kwani husaidia sana kuimarisha afya zetu.

Zifuatazo ni baadhi za faida ambazo huweza kuzipata mtu anayetumia nyanya mara kwa mara>>>

Matumizi ya nyanya husaidia sana kuweka mgonjwa katika mazingira mazuri ya kuepuka kukumbwa na tatizo la saratani, hii ni kutokana na kuwa na kirutubisho kiitwacho 'antioxidant' ndani yake.

Miongoni mwa aina za saratani ambazo utaepukana nazo kwa kutumia nyanya ni pamoja na saratani ya kibofu, tumbo, matiti na hata saratani ya mdomo hii ni kwa mujibu wa 'Harvard School of Pub Health'

Nyanya pia zinautajiri mkubwa wa kiwango cha vitamin C, madini ya chuma na potassium.

Potassium husaidia sana kuimarisha afya ya akili na kwa upande wa madini ya chuma yenyewe husaidia sana katika kuongeza damu mwilini, huku vitamin C ikiwa msaada wa kuimarisha kinga za mwili.

Vitamin A, pia hupatikana sana kwenye nyanya ambayo humsaidia mhusika anayetumia tunda hili kuongeza uwezo wake wa uoni na kuondosha shida ya kutoona vizuri usiku 'night blindness'

Aidha, matumizi ya nyanya pia husaidia kuimarisha afya ya mifupa, nywele, ngozi na meno hususani pale unapopata juisi ya nyanya yenyewe.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri zaidi. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.


No comments:

Post a Comment