Monday, 1 August 2016

Orodha ya vyakula na matunda muhimu kwa afya ya moyo


Binadam tunasumbuliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na magonjwa yasiyoambukizwa ambayo ni pamoja na shinikizo la damu.

Vifuatavyo ni baadhi ya vyakula ambavyo huweza kusaidia  kupunguza tatizo la shinikizo la damu

Nafaka
Kula nafaka, hasa nafaka zisizokobolewa na kutolewa viini, na zenye 'fiber'. Nafaka kama vile mahindi yasiyokobolewa au ngano, vinaweza kupunguza uwezekano wa kupata shinikizo la damu.

Mboga za majani
Mboga za majani nazo ni nzuri kwa watu wenye tatizo kama hili hususani spinachi au mchicha vina kalori kwa kiwango kidogo na nyuzinyuzi kwa wingi na ina virutubisho muhimu vya moyo kama potassium na magnesium ambayo ni madini muhimu kwa ajili ya kupunguza viwango vya shinikizo la damu.

Ndizi
Ndizi zimesheheni madini ya  potassium  kwa wingi huvyo nayo huweza kulinda afya ya moyo na kupunguza tatizo la shinikizo la damu.

Alizeti
Mbegu za alizeti pia ni chanzo kizuri cha madini ya magnesium ambayo husaidia kupunguza shinikizo la damu.
Zambarau, Kula kiasi kidogo cha zambarau kwa wiki kunaweza kusaidia kupunguza hatari ya shinikizo la damu.
Kwa ushauri zaidi tupigie kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment